Ubalozi wa Tanzania mjini Nairobi umeshiriki Onyesho la Kwanza la Utalii katika Jumuiya ya Afrika Mashariki lililofanyika kwenye viwanja vya TGT Arusha tarehe 9 - 11 October 2021. Onyesho hilo limewaunganisha Wanunuzi wa Huduma za Utalii na watoa huduma za utalii wakiwemo Mamlaka za Uhifadhi na Usimamizi wa Utalii, Tour Operstors, Wamiliki wa Hoteli, Wasafirishaji wa Watalii. Makampuni na taasisi za utalii zaidi ya 150 kutoka nchi za Afrika Mashariki yaani Tanzania, Kenya, Uganda, Sudani Kusini na Uganda yameshiriki maonyesho hayo, na wanunuzi kutoka nchi 19 wamehudhuria!
Katika Jumuiya ya Afrika Mashariki Tanzania na Kenya ndio nchi zenye ushirikiano mkubwa katika masuala ya utalii. Onyesho lilifungwa rasmi tarehe 11 Oktoba 2021 na Mheshimiwa Dkt. Hussein Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.