Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko (Mb) akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA). Mhe. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati anatarajia kushiriki Mkutano wa Pili wa Masuala ya Nishati ya Nyuklia kati ya Marekani nan chi za Afrika (US-Africa Nuclear Energy Summit) utakaofanyika atrehe 29 -30 Agosti, 2024 jijini Nairobi. 

Mkutano huu utahusisha majadiliano kuhusu Sekta ya Nishati kuongeza mnyororo wa thamani kwa ajili ya uendelezaji wa nyuklia pamoja na umuhimu wa kuwashirikisha wanawake na vijana katika Sekta ya Nishati. 

  • Mhe. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati akisalimiana na Mhe. Dkt. Bernard Kibesse, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Kenya mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA), tarehe 28 Agosti, 2024
  • Mhe. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati akipata maelezo kutoka kwa Mhe. Dkt. Bernard Kibesse, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Kenya mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA), tarehe 28 Agosti, 2024
  • Mhe. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati katika mazungumzo na Mhe. Dkt. Bernard Kibesse, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Kenya mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA), tarehe 28 Agosti, 2024