Tarehe 15.7.2021 Balozi wa Tanzania ambaye yupo accredited nchini Eritrea aliwasilisha Hati za utambulisho kwa Rais Mhe Isaias Afwerki katika jengo la ofisi maalum ya Rais anapofanyia shughuli za kidiplomasia mjini Asmara,Eritrea

Wakati wa kuwasilisha Hati Balozi Mhe Dkt John Simbachawene alimpatia salam kutoka kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan.na alimhakikishia kuboresha zaidi mahusiano kati ya Tanzania na Eritrea.