Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amehutubia Mabunge Mawili ya Kenya (Bunge la Taifa pamoja na Bunge la Senate la Kenya) Jijini Nairobi tarehe 05, Mei, 2021.

Akiwahutubia wabunge hao wa Mabunge hayo ya Kenya Mhe. Rais Samia amewataka kuendeleza udugu wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na Kenya.

Amesema Tanzania na Kenya ni ndugu wa siku nyingi udugu ambaoo utaendelea kuwepo siku zote na ndio maana hata wanyama aina ya nyumbu huishi kwa kuhama kati ya Kenya na Tanzania kama mzunguko wa maisha yao

Mhe. Rais Samia alikuwa nchini Kenya kwa ziara rasmi ya kiserikali ya siku mbili kufuatia mwaliko wa mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru. Kenyatta.