Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ambae yuko nchini Kenya kwa ziara rasmi amesema yuko nchini Kenya kwa ajili ya kuimarisha uhusiano mzuri ambao umekuwa tangu kitambo baina ya nchi hizi mbili.

Dkt Magufuli ambaye uongozi wake umepongezwa na wengi baada ya kupigana na rushwa,alisema yuko Nairobi ili kueleza kuhusu sera zake ambazo zinaifanya Tanzania kuwa sehemu nzuri ya uwekezaji.

Aidha Magufuli alisema kwamba amemhakikishia Rais Kenyatta kwamba Kenya mwenza nambari moja wa kibiashara wa Tanzania,na kueleza kuwa kuna makampuni mengi ya Kenya nchini Tanzania kuliko taifa lolote la Afrika.

Alisema Tanzania inawakaribisha wakenya wote ambao wanataka kufanya biashara jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake Rais Uhuru Kenyatta alisema Kenya na Tanzania zimekuwa na uhusiano mwema tangu miaka ya kitambo.

Aidha Kenyatta alisema kuwa Kenya na Tanzania ni baadhi ya nchi chache za Afrika ambazo zimekuwa na mabadiliko ya serikali kwa njia ya demokrasia na amani.

Rais Uhuru Kenyatta alisema Mawaziri wan chi za nje wa Kenya na Tanzania watapanga kamisheni ya pamoja ambayo itakutana nchini Tanzania hivi karibuni na kupanga utekelezaji wa kazi ambazo serikali hizo mbili zitakuwa zinafanya.

Pia alisema walijadiliana kuhusu matatizo ya nchi za Afrika mashariki.

  • Rais Dkt John Pombe Magufuli, akilakiwa na Mwenyeji wake, Rais wa Kenya, Mh. Uhuru Kenyatta alipokaribishwa Ikulu, Nairobi nchini Kenya leo. Rais Magufuli yupo nchini Kenya kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.Rais Dkt John Pombe Magufuli, akilakiwa na Mwenyeji wake, Rais wa Kenya, Mh. Uhuru Kenyatta alipokaribishwa Ikulu, Nairobi nchini Kenya leo. Rais Magufuli yupo nchini Kenya kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
  • Rais Dkt John Pombe Magufuli (kulia) akiwa na Mwenyeji wake, Rais wa Kenya, Mh. Uhuru Kenyatta wakipokea salamu za kijeshi, katika viwanja vya Ikulu ya Kenya, Jijini Nairobi leo.Rais Dkt John Pombe Magufuli (kulia) akiwa na Mwenyeji wake, Rais wa Kenya, Mh. Uhuru Kenyatta wakipokea salamu za kijeshi, katika viwanja vya Ikulu ya Kenya, Jijini Nairobi leo.
  • Rais Dkt John Pombe Magufuli akikagua gwaride la Jeshi la Kenya, alipowasili Ikulu jijini Nairobi leo.Rais Dkt John Pombe Magufuli akikagua gwaride la Jeshi la Kenya, alipowasili Ikulu jijini Nairobi leo.
  • Rais Dkt John Pombe Magufuli akikagua gwaride la Jeshi la Kenya, alipowasili Ikulu jijini Nairobi leo.Rais Dkt John Pombe Magufuli akikagua gwaride la Jeshi la Kenya, alipowasili Ikulu jijini Nairobi leo.
  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mbalimbali wa Kenya mara baada ya kumaliza  mazungumzo yao na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mbalimbali wa Kenya mara baada ya kumaliza mazungumzo yao na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.
  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na ujumbe wake katika mazungumzo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na ujumbe wake katika Ikulu ya Nairobi.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na ujumbe wake katika mazungumzo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na ujumbe wake katika Ikulu ya Nairobi.