Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. John Simbachawene alikutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kazi na Hifadhi za jamii wa Kenya Mhe Simon Chelugui katika ofisi za Wizara hiyo zilizopo katika jengo la Nssf jijini Nairobi. Mazungumzo hayo yalihusu kuboresha mahusiano katika masuala ya kazi na hifadhi za jamii kati ya Tanzania na Kenya. Kikao hicho pia  kilihudhuriwa  na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ndugu Peter K.Tum.