Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu atembelee Ofisi za Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Kenya.

Katika ziara hiyo, Mhe. Waziri Sangu alipata fursa ya kuonana na watumishi na kupata maelezo mafupi kuhusu kazi zinazofanywa na Ubalozi katika kutekeleza Sera ya Mambo ya Nje ya Diplomasia ya Uchumi.

Aidha, Mhe. Waziri alipongeza Ubalozi kwa kazi nzuri inayofanya na kuhimizi kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi na kusimamia maslahi ya Tanzania nchini Kenya.