Naibu Waziri,Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Reuben Kwagilwa (Mb.) ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 24 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria uliofanyika leo, tarehe 23 Oktoba, 2026, Kisumu, Kenya. Mkutano huu ulitanguliwa na Mkutano wa Ngazi ya Maafisa Waandamizi na ule wa Ngazi ya Makatibu Wakuu kuanzia tarehe 19 hadi 22 Oktoba, 2026.
Katika Mkutano huo, serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilipongezwa kwa uamuzi wake wa kupeleka Meli mpya ya MV New Mwanza inayotarajia kuanza safari zake katika Xiea Victoria. 
Mbali na Mkutano huu, ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayesimamia masuala ya Afrika Mashariki, Bw. Charles Ngeleje Kadonya ulipata fursa ya kutembelea Bandari ya Kisumu ili kubadilishana uzoefu na pia kujadili ujio wa Meli ya MV New Mwanza inayotarajia kuanza safari zake hivi karibuni katika Bandari hiyo.
Karika ziara hiyo, pamoja na mambo mengine, Katibu Mkuu alisisitiza umuhimu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashiriki kuendelea kushirikiana katika kuhakikisha matumizi ya Ziwa Victoria yanakuwa yale yenye kuleta maendeleo endelevu na tija kwa nchi zote wanachama huku tukihakikisha ulinzi wa mazingira. Aidha, aliishukuru serikali ya Kenya kwa ushirikiano inaoutoa katika kuhakikisha Meli ya MV New Mwanza inaanza safari zake katika Bandari ya Kisumu.