Katika hatua nyingine, Mhe. Waziri Deus Sangu alitembelea pia mradi wa kimkakati wa ujenzi wa Majengo Pacha ya Kitegauchumi unaotekelezwa kwa makubaliano kati ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Kwa mara nyingine tena Mhe. Waziri aliipongeza Wizara ya Mambo ya Nje kupita Ubalozi wake, kwa kuendelea kusimamia utekelezaji wa mradi huo ambapo kwa sasa umefikia asilimia 32.45 ya utekelezaji huku ukitarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2028.