Wajumbe wa Kamati ya Bajeti ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mheshimiwa Mashimba Ndaki, pamoja na Mhe. Masanja Kadogosa (Mb), Waziri wa Ujenzi wamekagua Maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la Ubalozi wa Tanzania , Nairobi

Ujumbe huo umepokelewa na Mheshimiwa Dkt. Bernard Y. Kibesse, Balozi wa Tanzania nchini Kenya, ambaye amewapatia taarifa kuhusu maendeleo ya mradi huo, hatua zilizofikiwa pamoja na umuhimu wa jengo hilo katika kuimarisha utekelezaji wa majukumu ya kidiplomasia na uwakilishi wa Tanzania nchini Kenya.

Ziara hiyo imewapa Wajumbe wa Kamati hiyo fursa ya kujionea maendeleo ya mradi na kutathmini uwekezaji unaofanywa na Serikali katika kuboresha miundombinu ya kidiplomasia, kuongeza ufanisi wa utendaji wa Ubalozi na kuimarisha taswira ya Tanzania kimataifa.